Sep 5, 2013

HURUMA!!! NDUGU WA BILIONEA ERASTO MSUYA ALIYEUAWA ARUSHA WAZIMIA MAHAKAMANI BAADA YA KESI..... FUATILIA


Ndugu wa mfanyabiashara Erasto Msuya (43)aliyeuawa kwa kupigwa risasi Agosti 7, mwaka huu, wameangua kilio na kuzimia  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Moshi, Kilimanjaro baada ya mahakama kuhairisha usikilizaji wa kesi hiyo.

Ndugu hao  ni dada wa marehemu, Antuja Msuya na Bahati Msuya ambao katika tukio hilo, wote  walipoteza fahamu.


Hali hiyo ilijitokeza baada ya mahakama kuahirisha kesi hiyo kufuatia maelezo ya upande wa mashtaka kuwa upelelezi haujakamilika na hivyo kuzua simazi na majonzi miongoni mwa watu waliohudhuria usikilizaji wa kesi.Wakili wa Serikali Stella

Majaliwa, aliomba mahakama kuridhia hoja ya kuahirisha shauri hilo ili kutoa nafasi ya kukamilisha shughuli za upelelezi.


Watuhumiwa walifikishwa mahakamani saa 5: 10, wakiwa ndani ya karandika la polisi.


Washtakiwa hao ni Sharifu Mohammed (31), mkazi wa Kimandolu mkoani Arusha, na Musa Mangu (38), mkazi wa Shangarai kwa Mrefu jijini Arusha.


Wanatuhumiwa kumuua Msuya kwa kukusudia, kinyume cha kifungu cha sheria namba 196 cha kanuni ya sura 16 ya mwaka 2012. Hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Theotimus Swai, aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 18 mwaka huu.


Mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo Shaiba Mpunga, hakuwepo mahakamani kwa kile kilichoelezwa kuwa ana matatizo ya kiafya.


Mshtakiwa wa kwanza na wa tatu katika kesi hiyo wanatetewa na Wakili Hudson Ndusyepo.

PICHA  ZA  MATUKIO:
 Watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya bilionea wa madini Erasto Msuya,Sharifu Mohamed na Musa Mangu wakiwa mahakamani.
 Ndugu wa marehemu Erasto Msuya wakiwa mahakamani.
 Ndugu wa marehemu Erasto Msuya wakiwa mahakamani.
 Wakazi wa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha walifurika mahakamani kusikiliza kesi hiyo.
 Mtuhumiwa Sharifu Mohamed akiteta jambo na wakili wake Mhe. Hudson Ndusyepo mara baada ya kuhairishwa kwa kesi hiyo .
 Dada wa marehemu Msuya aliyefahamika kwa jina la Antuja Msuya baada ya  kupoteza fahamu mara baada ya kuahirishwa kwa kesi.
 Dada wa marehemu Msuya aliyefahamika kwa jina la Antuja Msuya baada ya kupoteza fahamu mara baada ya kuahirishwa kwa kesi.
 Dada wa marehemu Msuya aliyefahamika kwa jina la Antuja Msuya akiangua kilio na baadae kupoteza fahamu mara baada ya kuahirishwa kwa kesi.
 Mdogo wa marehemu Msuya aliyefahamika kwa jina la Bahati Msuya akiwa anasaidiwa kupelekwa kwenye gari mara baada ya kuahirishwa kwa kesi
hiyo.
 Mdogo wa marehemu Msuya aliyefahamika kwa jina la Bahati Msuya akiwa anasaidiwa kupelekwa kwenye gari mara baada ya kuahirishwa kwa kesi
hiyo.
 Mama mzazi wa marehemu Erasto akisindikizwa na wanandugu kwenda kwenye gari la familia.
Umati mkubwa wa wananchi ulifurika mahakamani hapo

WHO IS ZARI: Born on the 23rd of September 1980. Zari grew up in a town called jinja in a country situated in east Africa known as Uganda, she attended her primary and later moved to Jinja girls high School where she thought to cultivate very positive personalities and passionate attitude towards achieving her dreams, on completion she moved to the city of kampala (The country capital city) where she performed karaoke in hang-outs during are vacation before she moved to London and acquired a diploma in cosmetology.
Music history: Zari started singing at early age in her primary days where she performed in musical concerts organized by her primary school staff, school’s end of the year functions and other community competitions representing her own school in shining colours. When she gained entrance into high school she joined the dance, drama and music groups which helped her score best actress for 2 consecutives years. After years of brilliant stage performances and school concerts, She took a break after moving from Uganda to London and continued with her studies but still with the compelling passion of music on her mind.
paparaziblog
TUPE MAONI YAKO TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE!!!.
WAIONAJE HII...TUPIA MAONI YAKO HAPA!
Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More